Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amevunja Baraza la Mawaziri pamoja na kumsimamisha kazi Makamu wa Rais Machar

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amelivunja Baraza lake la Mawaziri na kumsimamisha kazi Makamu wa Rais Riek Machar tukio ambalo linatajwa kuwa kubwa zaidi kufanywa na Kiongozi huyo katika kipindi cha miaka miwili tangu Taifa hilo lijipatie uhuru wake kutoka Sudan.


Kiongozi huyo wa Sudan Kusini amevunja Baraza lake la Mawaziri akiwa na lengo la kufanya mabadiliko makubwa ndani ya Serikali ya Juba baada ya kufanya tathmini ya Uongozi wa kipindi cha miaka miwili ambapo ameona kuna masuala hayajafanyika ipasavyo.
Waziri wa zamani wa Habari na aliyekuwa Msemaji wa Serikali Barnaba Marial Benjamin ndiye amethibitisha hatua hiyo ya kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri na kusimamishwa kazi kwa Makamu wa Rais Machar.
Mabadiliko hayo ya Rais Kiir hakauishia kwa Makamu wa Rais Machar pekee bali yalielekea hadi ndani ya Chama Tawala cha SPLM ambapo Katibu Mkuu Pagan Amum naye amekumbwa na wimbi hilo la mabadiliko.
Benjamin ambaye amesalia kuwa Mbunge pekee na si Waziri wa Habari na Msemaji wa Serikali amesema kile ambacho kimefanywa na Rais Kiir kipo kwa mujibu wa sheria na katiba ya Taifa hilo na ana mamlaka ya kuweza kuunda serikali nyingine.
Mawaziri wengine ambao walikuwepo kwenye Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Juba ni wale ambao walikuwa waasi kupitia SPLM na ambao walikuwa mstari wa mbele kukabiliana na ukatili ulioanza mwaka 1983 hadi 2005.
Sababu kubwa ambayo inatajwa kumsukuma Rais Kiir kuchukua uamuzi huo ni uwepo wa mgogoro wa kisiasa katika Taifa hilo na umechochewa zaidi ya hatua ya Makamu wa Rais Machar kutangaza nia yake ya kuwania Urais kwenye uchaguzi ujao.
Tayari Jeshi limewatawanya wanajeshi wa kutosha kwenye mitaa mbalimbali ya Jiji la Juba kuhakikisha hali ya usalama inaendelea kuimarika kwani kumekuwa na hofu ya huenda kukazuka machafuko.
Katibu Mkuu aliyetimuliwa wa Chama Cha SPLM Amum amekiri kupata taarifa za yeye kuondolewa kwenye wadhifa wake na kusema uamuzi huo umechukuliwa kutokana na sababu nyingi ambazo hakutana kuziweka bayana.
Tayari Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza imetoa onyo kwa Serikali ya Juba kuwa makini na uamuzi wake kwani hatua hiyo inaweza ikaongeza mgogoro wa kisiasa ambao ukachangia taifa hilo kuingia kwenye machafuko.

SOURCE rfi

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amevunja Baraza la Mawaziri pamoja na kumsimamisha kazi Makamu wa Rais Machar Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amevunja Baraza la Mawaziri pamoja na kumsimamisha kazi Makamu wa Rais Machar Reviewed by Tunchi Montana on July 24, 2013 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.