Raia wawili wa Uingereza wamwagiwa tindi kali visiwani Zanzibar nchini Tanzania

Raia wawili wa Uingereza wamemwagiwa tindi kali nchini Tanzania kwenye eneo la mji wa mkongwe visiwani Zanzibar "Stone Town" na sasa wamesafirishwa hadi jijini Dar es Salaam Tanzania bara kwa matibabu zaidi, polisi wamesema.

Raia hao wawili wasichana wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 wanaaminika kuwa walikuwa wakifanya kazi za kujitolea visiwani humo na kwamba tukio hili ni la kwanza kufanywa kwa raia wa Kigeni.
Kaimu kamanda wa Polisi Visiwani Zanzibar, Mkadam Khamis amewaambia waandishi wa habari visiwani humo kuwa watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki waliwakaribia wasichana hao na kisha kuwamwagia tindi kali.
Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania imekiri kuwa na taarifa hizo na kwamba wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha raia hao wanapatiwa matibabu ya haraka kuwanusuru na madhara zaidi ya acid hiyo.
Polisi wanasema bado wanaendelea na uchunguzi na kwamba mpaka sasa watu waliohusika na shambulio hilo hawajafahamika ila uchunguzi bado unaendelea na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kubaini wahusika.
Wizara ya mambo ya nje imesema kuwa zaidi ya raia elfu 75 wa Uingereza ambao huetembeala Tanzania kila mwaka, hivi karibuni kumekuwa na mashambulizi yakuwalenga raia wakigeni jambo ambalo linahatarisha usalama wao.
Wizara hiyo imeongeza kuwa kumekuwa na matukio ya uporaji wa mizigo ya raia wa kigeni hasa kwenye baadhi ya mitaa ya jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine hali ambayo hivi sasa inaonekana kuota mizizi.
Hivi Karibuni watu wasiofahamika walimwagia tindi kali mufti msaidizi wa Zanzibar pamoja na kumpiga risasi padri wa kanisa Katoliki.

source:RFI
Raia wawili wa Uingereza wamwagiwa tindi kali visiwani Zanzibar nchini Tanzania Raia wawili wa Uingereza wamwagiwa tindi kali visiwani Zanzibar nchini Tanzania Reviewed by Tunchi Montana on August 08, 2013 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.